Ijumaa, 16 Machi 2018

Mwalimu aliyefundisha kompyuta ubaoni aalikwa na Microsoft


Je, unakumbuka picha za mwalimu huyu,Owura Kwadwo.
Mafunzo ya kompyuta bila kwa njia ya ubao

Mafunzo ya kompyuta bila kwa njia ya ubao
Mwezi uliopita mwalimu huyu alivuma mtandaoni baada ya kuweka picha akichora programu ya Microsoft Word kwenye ubao wakati wa darasa la tarakilishi.
Mwalimu aliyefundisha darasa la kompyuta kwa njia ya Ubao azawadiwa
Iligundulika kwamba alifanya hivyo kwa sababu shule anayofundishia haikuwa na tarakilishi za kuwafundushia wanafunzi somo hilo la kompyuta.
Alisema "kufundisha somo la kompyuta nchini Ghana inachekesha.
Sasa mwalimu huyo anahudhuria mkutano wa walelimishaji wa Microsoft unaofanyikia nchini Singapore.
 Ujumbe wa Twitter wa @MicrosoftAfrica: BREAKING NEWS We're excited to see Owura Kwadwo Hottish in Singapore attending the Microsoft Global Education Exchange Summit! Hakimiliki @MICROSOFTAFRICA
Ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, "Nimefika nchini Singapore katika mkutani wa Microsoft Global Education Exchange, Ninatarajia kujifunza mengi. Asante Microsoft.
Baada ya picha yake Owura Kwadwo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, kampuni ya Microsoft ilivutiwa na mwalimu huyo na kumpatia msaada wa vifaa vya kumsaidia katika kazi yake.
Usisahau ku share Facebook,  TwitterInstagram

Jumamosi, 10 Machi 2018

Website za ku-download movies na series bure kwa kutumia simu yako hizi apa

Website hizi unaweza ku-download movies na series kwa kutumia simu yako ya kiganjani hata computer pia unaweza ku-download pia

WEBSITE ZA MOVIES
Hapa tutaanza na website za ku-download movie kwa sababu watu wengi wamekuwa wakisumbuka jinsi ya ku-download movie kwenya simu hizi apa sasa
(bonyeza maneno ya rangi ya blue kwenda kwenye website moja kwa moja) 
hapa utapata movies za kingereza mpya na za kihindi mpya kabisa. bonyeza hapo

Download hapo movies za kingereza na za kihindi quality

Download hapo movies za kingereza na za kihindi quality

WEBSITE ZA SERIES/SEASON ZA KINGEREZA
Hapa utapata series zote za kingereza kwa wakati kwa series zote kali za kingereza



Hizo apo ni website kali na za kuaminika za kudownloadia movie na series/season kali zinazo trend/hit zicheki alafu drop comments hapo usisahau ku share wenzako waone nao usiwe mchoyo

Ijumaa, 2 Machi 2018

TANZANIA: KIJANA WA MIAKA 17 ALIYEJEUZA TAKA ZA PLASTIKI KUWA MALIGHAFI

kijana Edga Edmund Tarimo aliyesimama hapo
Akiwa na umri mdogo tu chini ya miaka 17, Edgar Edmund Tarimo ameweza kubuni na kutengeneza mashine ya kutengenezea vigae vya sakafu, (Paving Blocks), kwa kutumia taka za plastiki na mchanga.
Kupitia ubunifu wake huo, ameweza kupunguza kiasi kikubwa cha taka za plastiki mitaani na kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira zinazotokana na taka hizo.
Na Kupitia kampuni yake ya Green Venture tayari ameajiri wafanyakazi sita na kuweza kutoa kipato kwa takriban watu themanini, ambao hufanya kazi ya kumkusanyia taka za plastiki.
Edgar anasema alianza ujasiriamali akiwa na mtaji wa shilingi za Kitanzania elfu 40, na tayari ameweza kushika mpaka kiasi cha milioni nne za Kitanzania.
Mkewe Obama amtambua mbunifu kutoka Kenya
Mbunifu wa mtambo wa Umeme asiyekuwa na elimu nchini Tanzania
Edgar Edmund ambaye amehitimu kidato cha nne mkoani Arusha mwaka uliopita, alikanza kutengeneza mashine hiyo aliyoivumbua miaka mitatu iliyopita, kutokana tatizo la mafuriko lililowahi kutokea na baadhi ya watu nyumba zao zilisombwa na maji, kutokana na kuokuwa imara na pia uchafu wa plastiki ulikuwa ukiathiri mazingira, kutokana na kusombwa na kutawanywa na maji kutoka maeneo mbalimbali wakati wa mafuriko hayo.
''Nilifikiria jinsi ya kutatua matatizo mawili kwa suluhisho moja ndio nikafikiria jinsi gani naweza kutumia taka kutengeneza bidhaa za ujenzi ambazo zinaweza kuwa za bei rahisi ili watu watumie kujengea katika nyumba zao ziwe imara, na pia kupunguza uchafu wa mazingira kwa kukusanya taka hizo za plastiki na kuzitumia.''
Kabla ya kutengeneza mashine hiyo, alikuwa akitumia jiko la kawaida la mkaa na sufuria kuweza kuyeyusha plastiki hizo.
Binti shujaa mbunifu wa Emoji iliyo na Hijab
Kwa upande wa mama yake, Emiliana Tarimo anasema hakutegemea mwanae kufikia mafanikio hayo, kutokana na jinsi alivyoanza na changamoto alizokutana nazo.
Hata hivyo anasema kutokana na umri wake mdogo, anamshauri aendelee na masomo yake na kuhitimu vizuri, ili aweze kupata mafanikio zaidi ya kazi yake.
Ameiomba serikali kuweza kusaidia mtoto huyu, kutopoteza kipaji chake na kuweza kuilinda kazi yake hiyo, kutokana na umri wake mdogo, wa chini ya miaka 18.
Mwaka jana wa 2017, Edgar Edmund alifanikiwa kupata tuzo ya Anzisha Prize baada ya wazo lake la kibiashara la kubadilisha taka za plastiki, kuwa malighafi ya kutengenezea vigae (paving Blocks) kwa kuchanganya na mchanga, kushinda.