Jumapili, 18 Februari 2018

KWA NINI WATU HAWAENDELEI KIMAISHA NA KUBAKI KAMA WALIVYO SIKU ZOTE



-Kutojiamini
watu wengi hawajiamini kama wanaweza kufika mbali kutoka hapo walipo na kufika juu zaidi kimaisha na kiuwezo sababu ya jinsi hali ilivyo, lakini kumbuka kila lenye mwanzo lina mwisho lakini mwisho wake unakuja kwa jitihada zako mwenyewe.
-Kutokuwa na mipango isiyokamilika
Watu wengi wana mipango lakini wanaofanikisha mipango yao ni wachache, kwa sababu wanakuwa hawana uvumilivu na maamuzi magumu ya kwamba hata chochote kutokee lazima ile mipango itimie. lakini watu mipango inaishaga kwa sababu ndogo na zisizo na maana. kama umeweka fedha kiasi fulani kwa kitu fulani hakikisha unafanikisha hata kitokee chochote.
-Kufuatia jinsi watu wanavyoishi na wewe uishi hivyo
kila mtu anaishi maisha yake mwenyewe na ya kitofauti. watu wamekuwa wakitaka kuishi maisha ya kitajiri angali wao ni watu wa maisha ya kawaida na hao wamejikuta wakijijazia matumizi yasiyo na maana na faida katika maisha yao na kubakia kama walivyo siku zote.
-Kukata tamaa/kuvunjika moyo
kukatw twmaa ni kitu kibaya sana. watu hukata tamaa pale wanaposhindwa kufanya kitu kwa mara nyingi. lakini kumbuka "unapofeli ndipo ushindi wako umekaribia" kwahiyo usikate tamaa kwa sababu kila jambo unalopitia lina faida mbeleni kwa sababu kuna unalo jifunza. USIKATE TAMAA.
-NOTE
kumbuka
                Mtajiri wanawekeza miradi (assets)
                Watu wa kawaida wanawekeza madeni (liabilities)
                Masikini wanawekeza matumizi (expenses)
   - Kama unataka kuendelea fanya kama tajiri wekeza miradi (assets) na sio uishi kama tajiri. asante kwa kusoma
Kama una ushauri na chochote kile weka comment yako hapo

Maoni 1 :

thank you